Nigeria: Wasichana wawili wa Chibok waliotekwa nyara waachiliwa huru miaka minane baadae
Makumi ya wanamgambo wa Boko Haram walivamia shule ya bweni ya wasichana ya Chibok mwaka 2014 na kuwapakia wanafunzi 276, wenye umri wa miaka 12-17, wakati huo kwenye lori katika tukio la kwanza la utekaji nyara wa shule ya halaiki ya kundi hilo la kijihadi.