Kundi la Taliban limeamuru shule za sekondari za wasichana zifungwe nchini Afghanistan, saa chache tu baada ya kufunguliwa tena.
Msemaji wa Taliban, Inamullah Samangani amethibitisha kuwa shule hizo kweli zimefungwa na wanafunzi wa kike wameamriwa kurudi nyumbani, hadi taarifa nyingine itakapotolewa.
Hajaelezea mara moja kuhusu hatua hiyo, ingawa msemaji wa Wizara ya Elimu, Aziz Ahmad Rayan amesema hawaruhusuwi kutoa maoni yao kuhusu suala hilo. Wanafunzi hao leo wamerudi shule kwa mara ya kwanza tangu Taliban ilipochukua madaraka mwezi Agosti mwaka uliopita.
Wakati huo huo, sare za shule kwa wasichana zinapaswa kushonwa kwa kuzingatia sheria ya dini ya Kiislamu, utamaduni na mila za Afghanistan.
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Afghanistan, Deborah Lyons amesema tarifa za kufungwa shule za wasichana Afghanistan zinaleta