Muda mfupi baada ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kutangaza kuwa mifumo ya Luku itazimwa kwa takribani siku 4 ili kufanya matengenezo kwenye kanzidata ya mfumo huo, matengenezo hayo yamesitishwa.
Taarifa iliyotolewa asubuhi ya leo Jumatano na Meneja Mwandamizi wa Tehama wa shirika hilo, Cliff Maregeli alisema matengenezo hayo ya siku nne yalikuwa yaanze Agosti 22 – 25, 2022 kuanzia saa 4 usiku hadi saa 1 asubuhi.
Kwa mujibu wa Tanesco ni kwamba matengenezo hayo yatafanyika hadi pale taarifa itakapotolewa tena