Wanafunzi wa darasa la saba wanaenda kuhitimisha elimu yao ya msingi hapo kesho, jumla ya watahiniwa 1,384,340 wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi utakaofanyika Oktoba 5 na 6 mwaka huu.
Kati ya watahiniwa hao 723,064 ni sawa na asilimia 52.23 ni wasichana na watahiniwa 661,276 sawa na asilimia 47.77 ni wavulana.
Asilimia 95.74 ya watahiniwa hao sawa na 1,325,433 watafanya mtihani kwa lugha ya Kiswahili na watahiniwa 58,907 sawa na asilimia 4.26 watafanya kwa lugha ya Kiingereza.Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) amezungumza na Waandishi wa Habari leo Actoba 04, Athuman Amasi ameeleza kuwa maandalizi yote ya mtihani huo yameshakamilika na amezitaka kamati za mitihani za mikoa na halmashauri kuhakikisha taratibu zinazingatiwa.
Pia amezielekeza kamati hizo kuhakikisha usalama wa vituo vya kufanyia mtihani unaimarishwa na vinazingatia mwongozo uliotolewa na baraza hilo.