Hii ni baada ya Sheikh Ponda kutoa taarifa kupitia ukurasa wa Twitter ikisema “22.03.2023 Jaji Mfawidhi alitembelea Mahabusu wa Ugaidi Arusha na kuwaambia kesi zao zimekwama kwa sababu Mahakama haijapewa Bajeti”
Mahakama imesema “Kufuatia taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya Kijamii kuwa mashauri ya watuhumiwa wa Ugaidi haijasikilizwa kwa sababu ya Mahakam kukosa bajeti, taarifa hiyo si ya kweli na inalenga kupotosha.
Tunapenda Umma ufahamu kuwa hakuna kuwa hakuna kauli ya namna hiyo ambayo imetolewa na Jaji Mfawidhi au kiongozi yeyote wa Mahakama, aidha suala la bajeti haliwezi kuhusishwa na Mahakama kwani bajeti ya kuita mashahidi inasimamiwa na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na sio Mahakama. Kwa hiyo hata anayesambaza taarifa hizo haelewi mgawanyiko ulivyo kuhusu jukumu la Mahakama katika jambo hili.
Kinachosikitisha zaidi ni kwamba upotoshaji huu unafanywa na Watanzania wenzetu, ni wazi kuwa kwa aliyetoa taarifa hizo za upotoshaji hana nia njema na Mhimili wa Mahakama.
Tunaomba Watanzania na wadau wa mnyororo wa haki, kupuuzia taarifa hiyo na kwamba haina ukweli wowote zaidi ya nia ovu yenye lengo la kuchafua taswira ya Mhimili wa Mahakama” imetolewa na Artemony T. Vincent, Mkurugenzi wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano.