Tanzania yaikana ripoti ya awali ya ajali ya ndege Bukoba

Serikali ya Tanzania imekanusha taarifa ya uchunguzi wa ajali ya ndege ya kampuni ya Precision Air iliyotokea Novemba 6, 2022 huko Bukoba na kusema taarifa hiyo ipuuzwe kwa kuwa haijatoka  katika mamlaka rasmi za Serikali.

Taarifa ya kanusho juu ya ripoti hiyo ambayo imesambaa mitandaoni toka siku Jumanne November 22 na kuripotiwa na vyombo mbalimbali vya ndani na nje ya Tanzania imekuja jana Novemba 23, wakati tayari imeshaibua mjadala mzito juu ya ajali hiyo.

Kwa mujibu wa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania ndugu Gerson Msigwa ni kwamba ripoti rasmi itatolewa itakapokuwa tayari na umma utataarifiwa.

Hata hivyo majibu hayo ya Msigwa yameibua mjadala na kupingwa na baadhi ya watu akiwemo mwanasiasa maarufu Zitto Kabwe kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT Wazalendo nchini Tanzania ambaye kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema yeye ni miongoni mwa walioisambaza taarifa hiyo na yuko tayari kupelekwa Mahakamani iwapo amesambazataarifa za uongo.

https://www.youtube.com/watch?v=y-oPDQcfPg8

Tangu ripoti hiyo inayodaiwa na Serikali kwamba si yao kutolewa na kuonyesha taarifa zinazotofautiana juu ya kijana Jackson Majaliwa aliyetajwa kama shujaa, kumekua na mjadala mkali wa maswali yanani aliyeokoa watu hao 24? Kwani ndani ya ripoti Majaliwa hakutajwa kama shujaa bali ripoti imeonyesha kuwa  muhudumu wa ndege na abiria ndio waliofungua mlango wa ndege kuokoa watu.

Itakumbukwa kuwa ripoti iliyotolewa ni ripoti ya awali lakini kwa sasa Serikali imebebeshwa mzigo wa lawama kwa kinachotajwa uzembe uliosababisha vifo vya waliokuwemo kwenye ndege hiyo.

https://mwanzotv.com/2022/11/23/ripotikuna-uzembe-ulifanyika-ajali-ya-ndege-bukoba/