Mfumo Tovuti ya tume ya uchaguzi ya Afrika Kusini imeonekana kuzimwaleo Ijumaa wakati nchi hiyo ikihesabu kura za uchaguzi mkuu ambapo chama tawala cha ANC kilionekana kupoteza wingi wake.
“Tunaomba radhi kwa suala hili na mfumo wetu wa NPE unaokabiliwa na changamoto, tunashughulikia kurejesha huduma,” tume hiyo ilisema.
“Mfumo wa matokeo bado unafanya kazi na ofisi za mitaa zinaendelea kuchukua matokeo”, ilisema.
Huku theluthi moja ya kura katika uchaguzi ikiwa imejumlishwa, ANC ilikuwa ikiongoza lakini ikiwa na alama ya asilimia 42 pekee chini ya asilimia 57 ilishinda mwaka wa 2019.
Muungano wa mrengo wa kati wa Democratic Alliance (DA) ulifuatia kwa asilimia 25. Chama cha mrengo wa kushoto cha Economic Freedom Fighters (EFF) na Mkhonto weSizwe (MK) cha rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma walikuwa shingo upande kwa takriban asilimia tisa kila mmoja.
Matokeo ya mwisho yanatarajiwa katika siku tatu zijazo.