Search
Close this search box.
Africa

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameitaka bodi mpya ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kufanya tafiti za dawa za saratani, ili kujibu maswali ya wananchi.

Amesema kumekuwa na maneno mitaani kuwa tunda la stafeli, linatibu saratani, hivyo muda wa wataalamu kujibu maswali hayo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, wakati akizindua bodi mpya ya taasisi hiyo, pia ameitaka kuweka mpango mkakati wa miaka 15 wa kufungua vituo vya saratani katika hospitali za Rufaa.

“Tunataka utafiti kuhusu dawa za saratani tunasikai stafeli inatibu saratani, tunataka wataalamu watafiti watuambie kama ni kweli tujue ni majani, au maganda tujue, hivyo watalaam mnisaidie kutifiti hizo dawa mje na ushahidi wa kisayansi kama zinatibu au hazitibu,”amesisitiza na kuongeza:

“Mjielekeze katika mafunzo na tafiti na muandae  mpango mkakati wa kufanya kwa miaka 15 katika Hospitali za rufaa, muweke senta huduma zenu zifike, muwe wadau wa saratani nchini nzima.”

Ummy ameitaka Ocean Road kujenga hostel kwa ajili ya ndugu wa wagonjwa au wagonjwa wanaotoka mikoani na kuweka mikakati maalum ya kuhakikisha huduma zinaendelea kuimarika.

Amesema wakati wa COVID-19, dawa asili zilisaidia kupambana na ugonjwa huo na tafiti zinaendelea.

Ummy amesema takribani watu 42,000 wanaugua ugonjwa wa saratani, huku ni wagonjwa 14,000 wanafika hospitali, hivyo wagonjwa wengi hawafiki.

Ameeleza kuwa kwa kila wagonjwa 100 kati yao 35 ni wanawake wanaougua saratani ya kizazi.

“Kwa wanaume asilimia sita wana  saratani ya tezi dume, kuna ogezeko mwaka 2018  walikuwa 150 na sasa hivi ni 531, inaweza ikawa tumeongeza huduma na sasa kuna kipimo.

“Watu wengi wanachelewa kufikia hospitali wanafika wakiwa steji ya nne ugonjwa umeshakuwa mkali, hivyo kuna haja ya kufanya uchunguzi wa saratani mapema na kuwaelimisha jamii kuhusu ugonjwa huo,” ameeleza.

Comments are closed