Waziri wa Afya nchini Tanzania, Ummy Mwalimu, amesema kirusi kipya cha Omicrom.DA 1, ambacho ni muunganiko wa virusi vya Delta na Omicrom bado hakijaingia nchini humo
Waziri Ummy aliyasema hayo leo jijini Dar es Salaam, wakati akipokea chanjo ya Covid-19 aina Sinovac dozi milioni moja kati ya milioni nne zilizoahidiwa kutolewa na Serikali ya Uturuki.
Ummy amesema kati ya sampuli 26 zilizochunguzwa, hakuna iliyopatikana na kirusi hicho kipya, huku shirika la Afya Duniani (WHO), likiendelea kuchunguza ukali wa kirusi hicho.
“Kirusi hicho kimeripotiwa katika mataifa mbalimbali, ambapo kwa Afrika nchi ya Afrika Kusini imethibitisha kuwa na kirusi hicho na sisi tunaendelea kusisitiza kuchukua tahadhari,” ameeleza Ummy.
Ummy amewataka wananchi kuendelea kupata chanjo, kwani ndio njia pekee ya kujikinga na kuchukua tahadhari zingine za kiafya.