Uuzaji asali isiyochakatwa nje ya nchi wapigwa marufuku.

Serikali ya Tanzania imezuia uuzaji wa asali isiyochakatwa kwenda  nje ya nchi ikisema uuzaji huo unaondoa thamani ya zao hilo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja ametoa marufuku hiyo leo wakati akizindua Programu ya Uwezeshaji na Mwongozo wa Ufuatiliaji Nyuki.

Amesema kwa sasa Tanzania ina viwanda vinavyotosha kuchakata asali yote inayozalishwa nchini.

Naibu Waziri Masanja amesema hata asali inayouzwa ndani ya nchi inapaswa kuchakatwa kwa ajili ya kuwekewa ubora unaotakiwa kwa watumiaji kuliko kuwauzia ilivyo.

Kuhusu programu hiyo, amewashuru Umoja wa Ulaya waliofadhili mradi huo kwa kutoka Euro 10 milioni ambayo ni sawa na Sh27 bilioni katika mikoa saba ikiwemo Tanzania Bara 5 na mikoa 

Amesema kuwa Serikali inalenga kuzalisha asali hadi tani 138,000 kwa mwaka ikiwa watu watahamasika na kuchangamkia mpango huo.

Amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na makatibu wakuu wengine kutenga maeneo ya ufugaji nyuki ili watu waweze kufuga kibiashara.

Balozi wa Umoja wa Ulaya, Manfredo Fanti amesema soko la asali kwa nchi za Ulaya ni kubwa na bado wanahitaji kiasi kikubwa kutoka Tanzania ndio maana wamewekeza fedha nyingi ambazo ni msaada na siyo mkopo.