Vijana 21 waliofariki kwenye mkanyagano nchini Afrika Kusini kuagwa leo

Afrika Kusini leo Jumatano itawaaga watu 21, wengi wao wakiwa vijana, waliofariki katika mazingira yasiyoeleweka katika tavern ya kitongoji mwezi uliopita, katika tukio ambalo lilishtua taifa hilo.

Rais Cyril Ramaphosa anatarajiwa kuhutubia ibada ya kumbukumbu ya wahasiriwa katika uwanja wa michezo katika kitongoji cha Scenery Park katika jiji la pwani la London Mashariki.

Kwa mujibu wa kamati ya mazishi ni kwamba Majeneza matupu yatawekwa, huku familia zikitarajiwa kuwazika watoto wao baadaye wiki hii.

Vijana hao walifariki katika kile ambacho walionusurika wamekitaja kuwa vita vya kutoroka ukumbi huo uliokuwa umejaa watu,kulikosababisha kukosekana kwa hewa ya Oksijen.

Mdogo zaidi alikuwa na umri wa miaka 14 na mkubwa zaidi 20, kulingana na tarehe za kuzaliwa zilizoorodheshwa kwenye programu rasmi ya ukumbusho iliyotolewa.

Waziri anayeshughulikia masuala ya usalama  Bheki Cele hapo awali alisema mdogo alikuwa na umri wa miaka 13 na mkubwa zaidi 17.

Vifo hivyo havikuwa na dalili zozote za kujeruhiwa na maafisa wamefutilia mbali mkanyagano kuwa chanzo cha vifo hivyo.

Uchunguzi wa polisi bado unaendelea.

Kunywa nchini Afrika Kusini kunaruhusiwa kwa zaidi ya miaka 18. Lakini katika tavern za mijini, ambazo mara nyingi ziko karibu na nyumba za familia, kanuni za usalama na sheria za umri wa kunywa hazitekelezwi kila wakati.

Nolitha Tsangani, mkazi wa Scenery Park anayeishi karibu na tavern ya Enyobeni ambako kisa hicho kilitokea, alisema lawama za mkasa huo zinapaswa kuhusishwa.

“Sote tunakosea… mzazi ana makosa, mtoto ambaye amekufa, nasikitika kusema, ana makosa,”