Vimbwanga vya wabunge wa Tanzania,Wengine walia na wengine waruka sarakasi bungeni

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeendelea na vikao vyake vya bajeti, ambapo hii leo Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amewasilisha bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Kizaazaa  kiliibuka bungeni baada ya wabunge waliokuwa wakichangia kufanya matukio yasiyo ya kawaida kuonesha kusikitishwa na utekelezaji wa miradi. 

Mbunge wa Ukonga, Jerry Slaa, ambaye alikuwa wa kwanza kuchangia mara baada ya bajeti hiyo kuwasilishwa na Waziri Profesa Makame Mbarawa, amejikuta akilia machozi kwa kile alichodai uchaguzi umekaribia huku utekelezaji wa miradi ya barabara ukiendelea kusuasua.

Mbunge huyo ambaye amewahi kuwa Meya wa Manispaa ya Ilala nchini Tanzania amesema kumekuwepo na wakandarasi ambao hawazingatii ubora wa barabara ikiwemo ile ya Mwendokasi ya Mbagala.

Akichangia hotuba hiyo Slaa amejikuta akilia machozi kwa kile alichodai uchaguzi umekaribia huku utekelezaji wa miradi ya barabara ukiendelea kusuasua.

Mbunge huyo ambaye amewahi kuwa Meya wa Manispaa ya Ilala amesema kumekuwepo na wakandarasi ambao hawazingatii ubora wa barabara ikiwemo ile ya Mwendokasi ya Mbagala.

Amesema tatizo hilo linatokana na makandarasi mmoja kupewa kazi zaidi ya nne aklitpolea mfano wa kampuni ya Sino-Hydro.

Amesema kampuni hiyo imesema mkandarasi huyo ana kazi sita ikiwemo ya ujenzi wa barabaraya mwendokasi kutoka Kariakoo-Mbagala.

“Mkandarasi huyo ambaye kilomita 25 zimekutwa na ufa, mkandrasi huyo amabye halipi wafanyakazi, asiyelipa wazabuni ameenda kuongezewa kazi nyingine,” amesema.

Ameongeza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan alishaonya kuhusu mkandarasi kupewa kazi nyingi lakini bado Sino Hydro ameendelea kupewa kazi nyingi.

Amesema kero hiyo inapelkwa tena kwa wananchi wa Gongo la Mboto kwa mkandarasi huyo kuendelewa kupewa tenda za ujenzi licha ya kutekeleza chini ya kiwango.

“Hatuwezi kuacha watu hawa wakaendelea kufanya kazi hiyo. Kuna jambo nilisema hapa kuhusu single source sio mbaya tatizo ni uadilifu wa wale wanaosimamia kazi hizi,” amesema.

Slaa kitaaluma ni mwanasheria amesema awamu ya kwanz aya mradi kutoka Kimara hadi Kivukoni ulijengwa na Kampuni ya Strabag “leo miaka saba hakuna shimo moa lililotopkea hivi wangempa phase iii single source Strabag kuna mtu angelalamika?”

Ametolea mfano mwingine wa mradi wa maji Arusha wenye awamu 13 ambapo alisema awamu 12 zimekamilika lakini awamu moja aliyopewa Sino-Hydro haijakamilika hadi sasa.

Mbali na Slaa Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay yeye amelazimika kupanda juu ya meza bungeni na kubinuka sarakasi kwa kile alichodai ni kuonesha kukasirika kwa jimbo lake kutojengwa barabara ya lami licha ya Serikali kuahidi katika kila bajeti.

Hii ni mara ya pili kwa mbunge huyo kutaka kupiga sarakasi baada ya Mei 17, 2021 akichangia bajeti ya Uchukuzi kutishia kufanya hivyo kabla ya Naibu Spika wakati huo Tulia Akson kumtaka asifanye hivyo.

Awamu hii ameamua kupiga sarakasi na kuahidi kushika shilingi ya Wizara hiyo endapo hatopewa majibu ya kuhusu ujenzi wa barabara ya lami jimbo la Mbulu Vijijini.

“Waananchi wa Mbulu hawajui barabara ya lami kabisa lakini hapa kuna barabara zingine zinakwenda kukarabatiwa ina maana hawa wameshakaa na barabara kwa muda mrefu na sasa zinaenda kuboreshwa,amesema Massay.

“Nimeonesha kuwa nimekasirika Mh. Waziri na nitakwenda kushika shilingi niende nayo kwa watu wa Mbulu,” amesema.

Kwa mujibu wa Waziri Mbarawa serikali imetekeleza bajeti ya miradi ya maendeleo sekta ya ujenzi kwa asilimia 96.5 yenye gharama ya Sh. 1.532 trilioni. ambapo hadi Aprili, 2022 fedha zilizopokelewa ni Sh. 1.532 sawa na asilimia 96.48 ya fedha zilizoidhinishwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2021/22. 

Sekta ya Ujenzi nchini Tanzania ilitengewa Sh 1.588 trilioni ikijumuisha Sh 1.288 fedha za ndani na Sh 300 milioni fedha za nje.

 Kati ya fedha zilizopokelewa Sh 1.232 trilioni ni fedha za ndani zinajumuisha Sh 691.1 milioni kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali na Sh. 541.6 milioni kutoka Mfuko wa Barabara na Sh 299.9 milioni ni fedha za nje.