Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania Prof Adolf Mkenda amepiga marufuku matumizi ya vitabu 16 vya ziada kutumika katika shule za umma na binafsi nchini humo.
Kwa mujibu wa sheria za Tanzania Waziri huyo amepewa mamlaka chini ya kifungu 59 cha sheria ya Elimu Sura 353 ambapo atakua na nguvu ya kutoa maamumzi chini ya sheria hiyo.
Vitabu hivyo16 vilivyopigwa marufuku vimekutwa katika baadhi ya shule si kama vitabu haya kiada wala ziada ambapo maudhii yake yanakizana na Mila, Desturi na Utamaduni wa Mtanzania na yanahatarisha ukuaji wa wanafunzi.
Waziri Mkenda amezitaka shule kufuata muongozo wa Waraka wa Elimu na kuwa vitabu vyote vya ziada vinavyo andikwa na waandishi binafsi vinatakiwa kuwa na ithibati ya ubora inayotolewa na Kamishna wa Elimu Tanzania.
Vitabu vilivyopingwa marufuku kutumika na kuwepo shuleni ni Diary of a Wimpy Kid, Diary of a Wimpy Kid -Rodrick Rules, Diary of Wimpy Kid – The Last Straw, Diary of Wimpy Kid-Dog Days, Diary of a Wimpy Kid The Ugly Truth, Diary of a Wimpy Kid -Cabin Fever.
Vingine ni Diary of a Wimpy Kid – The Third Wheel na Diary of a Wimpy Kid – Hard Luck, Diary of a Wimpy Kid – The Long Haul, Diary of a Wimpy Kid -Old School, Diary of a Wimpy Kid -Double Down, Diary of a Wimpy Kid-The Gateway, Diary, Diary of a Wimpy Kid-Diper Overlode, Is for TANSGENDER ( you know best who you are!), Is for LGBTQIA ( find the words that make you you) na Sex Education a Guide to life.
Marufuku hii imekuja siku kadhaa baada ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kumtaka Waziri huyo kuangalia namna ya uboreshaji wa mitaala shuleni ili kutoa elimu bora inayozingatia pia mila, tamaduni na desturi za Tanzania