Wagonjwa nane wa Ebola nchini Uganda waruhusiwa hospitali

Wagonjwa nane waliotibiwa  Ebola nchini Uganda wamepona, amesema waziri wa afya wa nchi hiyo Jumatano, akitangaza kuwa milipuko wa ugonjwa huu wa hatari umekwisha.

Waziri Jane Ruth Aceng amesema kuwa wagonjwa hao wanane walikuwa wakitibiwa na sasa wamepona kikamilifu.

Alisema wagonjwa walitolewa hospitalini Jumanne na Jumatano kutoka hospitali moja mjini Kampala.

Uganda ilikuwa imethibitisha kesi tisa kwa jumla katika milipuko ya hivi karibuni, ikiwemo nesi mmoja ambaye alifariki kutokana na ugonjwa huu katika mji mkuu, Kampala, Januari.

Aceng alisema kuwa watu 265 wengine bado wako “katika karantini kwa uangalizi” baada ya kuwa na mawasiliano na mgonjwa aliyefariki.

“Kwa sasa, maambukizi ya Ebola yamezuiwa kama sehemu ya hatua kali za serikali ya Uganda kutokomeza kuenea kwa magonjwa, pamoja na mashirika ya kimataifa, aliongeza.

Hii ni mara ya sita kwa taifa hili la Afrika Mashariki kuathiriwa na virusi vya Ebola ambavyo havina chanjo rasmi.

Jaribio la chanjo dhidi ya aina hii lilianzishwa nchini Uganda mapema mwezi huu.

Milipuko ya Ebola ya awali nchini Uganda ilidumu kwa miezi minne mwaka 2022 na 2023 na kuua watu 55.

Milipuko ya Ebola yenye vifo vingi zaidi ilitokea Afrika Magharibi kati ya mwaka 2013 na 2016, ikiwa imeua zaidi ya watu 11,300, kulingana na takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO).