WAMASAI WA NGORONGORO WAANDAMANA KUDAI HAKI ZAO IKIWEMO YA KUANDIKISHWA KAMA WAPIGA KURA

Jamii ya watu wa Kimaasai waishio Ngorongoro mapema leo asubuhi wameandamana kwa amani wakiishinikiza Serikali ya Tanzania kuheshimu haki zao za msingi ambazo wanadai zimepokwa na Serikali hiyo kwa takribani miaka minne sasa.

Wamasai waishio Ngorongoro kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na vizuizi vya huduma za kijamii, unyanyasaji wa kimwili na serikali, ukiukwaji wa haki za ardhi, kukataliwa kuandikishwa kama wapiga kura na kutakiwa kuhama na kadi za kupita katika ardhi yao wenyewe.

Wameanza maandamano hayo kwa kuweka Vizuizi vya barabara kuu, vilivyoanza saa kumi na mbili asubuhi ya leo Agosti 18, 2024.

Mara kwa mara Wamasai wametoa wito wa kutendewa haki, upatikanaji wa huduma za msingi, ulinzi wa ardhi yao, lakini hadi sasa Serikali ya Tanzania imeonekana kukaidi maombi ya Wamasai hao.

“Hatuzuii barabara hii kuu bila hiari tunafanya kwa lazima,” mwandamanaji mmoja alisema asubuhi ya leo kando ya barabara kuu. “Kwa muda mrefu sana, sauti zetu zimepuuzwa, na haki zetu zimekandamizwa,”

Jamii inazitaka mamlaka husika kufanya mazungumzo yenye maana ili kushughulikia matatizo yao. Pia wanatoa wito kwa umma kwa mapana kuelewa mazingira ya Wamasai na kuunga mkono vita vyao vya kupigania haki.

Kwa miaka minne iliyopita, serikali ya Tanzania imesimamisha huduma zote za kijamii kama afya na elimu katika eneo la Ngorongoro kama kichocheo cha Wamasai kuhama makazi yao