Wanawake wanne wamefariki dunia katika mkanyagano magharibi mwa Kenya leo Ijumaa baada ya umati wa watu kuogopa mlio uliotokana na kumwagika kwa chai ya muuzaji mmoja kwenye moto wakidhanini ni gesi ya kutoa machozi .
Kisa hicho kimetokea katika mji wa Kericho kilitokea nje ya uwanja ambapo Rais William Ruto alipaswa kutoa hotuba ya siku ya kitaifa saa kadhaa baadaye.
Mwanamke aliyekuwa akiuza chai aliiteketeza kwa bahati mbaya, huku watu wakisubiri alfajiri kuingia uwanjani.
“Kulikuwa na mkanyagano uliosababishwa na mwanamke aliyekuwa akiuza chai nje ya uwanja ambaye kwa bahati mbaya alimwaga chai ya moto kwenye moto karibu na lango C kando ya barabara ya umma,” walisema Polisi na kuongeza
“Matokeo yake wananchi waliingiwa na hofu na kudhani kuwa ni mabomu ya machozi yaliyorushwa kwao.”
Watu kadhaa walijeruhiwa na kupelekwa hospitalini, iliongeza.
“Katika hospitali hiyo, wanawake wanne ambao hawajatambuliwa wamethibitishwa kufariki.”
Matukio ya kuadhimisha Siku ya Mashujaa yaliendelea baadaye kama ilivyopangwa katika uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watu 10,000 ikijumuisha hotuba ya Ruto.
Sikukuu hiyo ni kwa heshima ya wale waliopigania uhuru ambao Kenya iliupata mwaka wa 1963.