Search
Close this search box.
Africa

Mamlaka ya Madagascar ilisema siku ya Jumatatu kuwa takriban watu milioni mbili wataathirika mara tu Kimbunga Freddy kitakapotua katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

Wataalamu kutoka Ofisi ya taifa ya Majanga wametabiri kuwa kimbunga hicho kitakumba mikoa tisa nchini huo.

Vikosi vya dharura vinajiandaa kukabiliana na mvua kubwa, mafuriko na hata maporomoko ya ardhi katika maeneo ambayo yataathiriwa.

Kimbunga hicho kimekuwa kikikumba bahari ya Hindi kwa wiki kadhaa na kwa mujibu wa wataalamu, athari zake zitaonekana kati ya wilaya za Vatomandry kusini-mashariki na Manakara ambayo iko pwani ya mashariki.

Wale wanaoishi katika maeneo hayo wameshauriwa kuimarisha milango na paa zao, kukata miti hatari na kubaki nyumbani wakati wa kimbunga hicho.

Taifa hilo la kisiwa ni miongoni mwa nchi 10 za juu zaidi barani Afrika zilizoathiriwa zaidi na vimbunga na hatari kwa majanga, kulingana na Mpango wa Chakula Duniani, Dhoruba la awali ya kitropiki iliyoikumba nchi ilikuwa Cheneso, iliyopiga Januari mwaka huu. Takriban watu 30 walikufa na zaidi ya 40,000 walikimbia makazi yao.

Comments are closed