Watumishi wa Umma nchini Tanzania waongezewa posho za safari.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Serikali ya Tanzania imetoa kibali cha kurekebishwa kwa posho ya kujikimu safarini kutosha shilingi 120,000 hadi shilingi 250,000 kwa daraja la juu na Sshilingi 80,000 hadi shilingi 100,000 kwa daraja la chini.

Taarifa hiyo imetolewa leo Ijumaa Mei 27, 2022 na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dk Laurean Ndumbaro.

“Rais Samia amebadilisha pia kiwango cha malipo cha kazi maalumu kwa ngazi ya chini kutoka shiling 15,000 hadi shilingi 30,000 kwa ngazi ya kazi kutoka shiling 20,000 hadi shiling 40,000 na ngazi ya juu kutoka shiling 30,000 hadi shiling 60,000”. amesema.

Dk Ndumbaro asema kuwa mabadiliko hayo yataanza rasmi Julai Mosi, 2021 na kwamba bajeti iliyopangwa ndiyo itakayotumika kutekeleza viwango hivyo.

Pia ametoa wito kwa wafanyakazi wa umma kufanya kazi kwa bidi zaidi bila kusubiri kusimamiwa, kujituma, kuwa wabunifu na wenye nidhamu na maarifa.