Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imeliagiza Jeshi la Polisi lianze kuwatafuta na kuwakamata wanaomiliki silaha kinyume cha sheria.
Pia Waziri wa wizara hiyo, Hamad Masauni ameliagiza jeshi hilo litumie taarifa ilizonazo kuwatafuta na kuwakamata wanaojihusisha kutengeneza magobore na lifanye mapitio ya sheria na kanuni ili kuona kama iko haja ya kuzifanyia marekebisho.
Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa silaha 301 zilisalimishwa kutoka mikoa 13 ya Tanzania Bara na mikoa mitatu ya kipolisi.
Ametaja mikoa iliyosalimisha kuwa ni Tanga ambayo silaha 138, Dodoma 76, Singida 19, Morogoro 18, Mkoa wa kipolisi Rufiji 12, Pwani 10, Songwe 9, Rukwa 6, Manyara 3, Mkoa wa kipolisi Kinondoni 3, Njombe 2, Geita 1, Arusha 1, Mkoa wa kipolisi Ilala 1, Mbeya 1 na Tabora 1.