Search
Close this search box.
Africa

Janga la UVIKO-19 liliua watu milioni 13.3 hadi 16.6 mnamo 2020 na 2021, WHO ilikadiria Alhamisi — hadi mara tatu ya idadi ya vifo vinavyohusishwa moja kwa moja na ugonjwa huo.

Makadirio ya Shirika la Afya Duniani yaliyosubiriwa kwa muda mrefu ya jumla ya vifo vilivyosababishwa na janga hilo — ikiwa ni pamoja na idadi ya wale waliopoteza maisha yao kutokana na athari zake – hatimaye idadi kamili ya athari ya janga hilo imejumuishwa.

“Makadirio mapya kutoka kwa Shirika la Afya Ulimwenguni yanaonyesha kuwa idadi kamili ya vifo iliyohusishwa moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja na janga la UVIKO-19 kati ya Januari 1, 2020 na Desemba 31, 2021 ilikuwa takriban milioni 14.9 (kuanzia milioni 13.3 hadi milioni 16.6),” WHO ilisema.

“Takwimu hizi muhimu sio tu zinaonyesha athari za janga hili lakini pia hitaji la nchi zote kuwekeza katika mifumo thabiti zaidi ya afya ambayo inaweza kudumisha huduma muhimu za kiafya wakati wa majanga,” Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema.

WHO ilitangaza Covid kuwa janga la kimataifa mnamo Januari 30, 2020, baada ya visa vya ugonjwa huo mpya kuenea nje ya Uchina.

Nchi nyingi kote ulimwenguni ziliripoti vifo milioni 5.42 vya UVIKO-19 kwa shirika la WHO mnamo 2020 na 2021 – idadi ambayo leo inafikia milioni 6.24, pamoja na vifo zaidi mnamo 2022.

Shirika hilo lenye makao yake makuu mjini Geneva limesema kwa muda mrefu idadi halisi ya vifo ilikuwa haijawekwa wazi.

Vifo vilivyohusishwa kwa njia isiyo ya moja kwa moja na janga hili vinatokana na hali zingine ambazo watu hawakuweza kupata matibabu kwa sababu mifumo ya afya ililemewa.

WHO ilisema kwamba vifo vingi vya ziada — asilimia 84 – vilitukia zaidi kusini mashariki mwa Asia, Ulaya na Amerika.

Nchi 10 pekee zilichangia asilimia 68 ya vifo vyote vya ziada.

Nchi za kipato cha juu zilichangia asilimia 15 ya vifo.

Mataifa ya kipato cha kati yalichangia vifo asilimia 28; mataifa ya kipato cha chini asilimia 53; na nchi zenye kipato cha chini asilimia nne.

Idadi ya vifo duniani ilikuwa juu zaidi kwa wanaume kuliko wanawake — asilimia 57 wanaume, asilimia 43 wanawake — na zaidi kati ya watu wazima wazee.

WHO ilisema idadi hiyo ya milioni 14.9 ilitolewa na wataalam wakuu duniani ambao walitengeneza mbinu ya kutoa makadirio pale ambapo data inakosekana.

Nchi nyingi hazina uwezo wa ufuatiliaji wa uhakika wa vifo na kwa hivyo hazitoi data inayohitajika kujumuisha viwango vya vifo vya ziada — lakini zinaweza kufanya hivyo kwa kutumia mbinu inayopatikana kwa umma.

WHO ilipaswa kufanya mkutano na waandishi wa habari baadaye Alhamisi kuelezea hesabu hiyo mpya.

Comments are closed