Mwanzo Tv

Nairobi Kenya

+254 7

24/7 Customer Support

Mon - Fri: 9:00 - 17:30

Online Media always open

WHO yatangaza chanjo ya malaria

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt. Tedros Ghebreyesus ametangaza pendekezo la shirika hilo la matumizi ya chanjo ya kwanza ya malaria ulimwenguni, ambapo ameeleza  kuwa chanjo hiyo iliyosubiriwa kwa muda mrefu ni mafanikio ya sayansi na afya ya mtoto dhidi ya malaria.

Chanjo hiyo imetangazwa kutokana na matokeo ya programu inayoendelea ya majaribio nchini Ghana, Kenya na Malawi ambayo imewafikia zaidi ya watoto 800,000 tangu mwaka 2019.

‚ÄúNdoto ya chanjo ya malaria imekuwa ndoto ya muda mrefu lakini isiyoweza kufikiwa. Leo, chanjo ya malaria ikifahamika kama RTS, S, zaidi ya miaka 30 ikifanyiwa utafiti¬†inabadilisha historia ya afya ya umma. Bado tuna barabara ndefu sana ya kusafiri. Lakini huu ni mserereko mrefu kuelekea chini kwenye barabara hiyo,‚ÄĚ amesema.Dkt. Tedros

Matokeo yameonesha kuwa ina uwezo wa kupambana na vimelea vya malaria kwa asilimia 30, na haina madhara kwa wanaotumia chanjo nyinginezo, au njia nyingine za kudhibiti malaria.

Ina uwezo wa kuzuia visa vinne kati ya 10 vya maambukizi ya Malaria na visa vitatu kati ya 10 vya madhara makubwa ya Malaria.

Thamani ya chanjo hiyo itaonekana zaidi barani Afrika, kwa sababu ndipo mzigo wa malaria ni mkubwa zaidi dunani.

Mbali na Malaria, chanjo hiyo ya kwanza imetajwa kuwa itapambana na ugonjwa wowote wa vimelea. kwa hivyo, itafungua fursa kwa magonjwa mengine pia katika udhibiti wa magonjwa mengine pia. 

WHO inapendekeza chanjo hiyo itumike kwa kuzuia malaria kwa watoto wanaoishi katika maeneo yenye maambukizi ya wastani hadi juu kwa vigezo vya WHO, na itolewe kwa mpangilio wa dozi 4 kwa watoto wa umri wa kuanzia miezi mitano.  

Malaria bado ni chanzo  kikuu cha magonjwa na vifo vya watoto katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara ambapo zaidi ya watoto 260,000 wa Kiafrika walio chini ya umri wa miaka mitano hufariki kutokana na ugonjwa huo kila mwaka.