Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Japani Shinzo Abe amefanyiwa mazishi ya kitaifa hii leo.
Abe aliyefariki akiwa na miaka 67, alikuwa waziri mkuu wa Japan aliyekaa muda mrefu zaidi na mmoja wa watu wanaotambulika sana kisiasa nchini humo, anayejulikana kwa kukuza ushirikiano wa kimataifa na mkakati wake wa kiuchumi wa “Abenomics”.