Tanzania na Marekani kushirikiana kibiashara kupitia Sekta binafsi
Serikali ya Tanzania imefungua milango ya ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi kati ya Tanzania na Marekani kupitia Sekta Binafsi ili kuchochea biashara kupitia uwekezaji ikiwa ni utekelezaji wa mazungumzo kati ya Marais wa nchi hizo mbili yaliyofanyika hivi karibuni mjini Washington DC.