Africa East Africa

UN Ripoti: Watu bilioni 2.3 wanategemea nishati chafu kupikia

Ripoti hiyo ya toleo la mwaka 2022 “Ufuatiliaji wa SDG 7: Ripoti ya Maendeleo ya Nishati” inaonyesha kuwa athari za janga hili, ikiwa ni pamoja na mashariti ya kufungwa kila kitu, kuathirika kwa minyororo ya usambazaji wa kimataifa, na upotoshaji wa rasilimali za kifedha ili kuweka bei za chakula na mafuta kuwa nafuu, vimeathiri kasi ya maendeleo kuelekea lengo la Maendeleo Endelevu SDG 7 la kuhakikisha upatikanaji wa nishati nafuu, ya kutegemewa, endelevu na ya kisasa ifikapo mwaka 2030.