Mwabukusi akosoa mkataba wa HGA, adai Serikali imewadanganya Wananchi, asisitiza maandamano
Mwabukusi ameeleza masikitiko yake kwa Serikali kusaini mkataba na DPW ya Dubai katika uendelezaji wa bandari ya Dar es Salaam akidai kuwa bado mapungufu hayajaondolewa na hata kipindi cha miaka 30 ya mkataba huo ni kirefu ikilinganishwa na raslimali inayoenda kuwekezwa.