Africa East Africa

Waziri Silaa kuburuzwa mahakamani kwa kuvunja nyumba ya Mahururu kinyume na sheria

Wakili wa kujitegemea Dikson Matata amesema wameweka nia ya kumfungilia kesi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa kwa kuvunja nyumba ya mteja wake kinyume na sheria.

Matata anamuwakilisha ndugu Johnsen Leornard Mahururu ambaye hivi karibuni amebomolewa nyumba yake ya ghorofa moja lililopo kwenye eneo la kiwanja no. 484 Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.