East Africa Rights & Freedoms Tanzania

ACT Wazalendo waionya Serikali kufungia mtandao wa X(Twitter)

Akiongea Jijini Dar es salaam leo June 12,2024, Waziri Kivuli wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa ACT Wazalendo, Rahma Mwita amesema Serikali ya CCM imekuwa na utamaduni wa kutovumilia maoni, mitazamo na fikra tofauti zinazotolewa na Wananchi kuhusu Viongozi na sera zao, na mara zote inatumia hila za namna tofautitofauti ili kutimiza dhamira hiyo kandamizi.