East Africa Politics Tanzania

Polisi wadaiwa kutumia nguvu ukamatwaji wa viongozi wa Chadema na wafuasi wake.

Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu Bara kutoka chama cha Chadema bwana Benson Kigaila ni kwamba katika kundi kubwa la watu takribani 500 waliokamatwa na Polisi kati ya siku hizo mbili, wakiwemo viongozi wakuu wa chama hicho ni kwamba Makamu Mwenyekiti Bara, Tundu Lissu, Katibu Mkuu John Mnyika na Mwenyekiti Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu wameumizwa vibaya kutokana na nguvu iliyotumika kuwakamata.