Africa Crime & Justice International Politics Rights & Freedoms

Masahibu ya Mpinzani Mkuu Wa Kagame, Victoire Ingabire! Kwa nini Kakamatwa?

Ingabire aliwahi kuhukumiwa kifungo cha miaka minane gerezani mwaka 2012 kwa makosa yaliyohusisha “kudharau mauaji ya kimbari” na “kutishia usalama wa taifa.” Hukumu hiyo ilitokana na hotuba aliyotoa aliporejea Rwanda kutoka uhamishoni, ambapo alitaka kutambuliwa pia kwa waathiriwa wa Kihutu waliouawa wakati wa mauaji hayo ya mwaka 1994.