East Africa Politics Tanzania

ACT Wazalendo yapinga uamuzi wa Msajili wa Vyama kuhusu mgombea wake wa urais

Katika taarifa yake kwa umma, chama hicho kimeeleza kuwa hatua ya Msajili haina mashiko ya kisheria kwa kuwa mchakato wa uchaguzi tayari umeshaanza, huku Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ikiwagawia wagombea fomu za kugombea urais. Kwa mujibu wa ACT Wazalendo, Msajili hana mamlaka ya kuingilia hatua hiyo, zaidi ya kushughulikia malalamiko kwa njia ya pingamizi.