SHAHIDI: SITAWARUHUSU VIONGOZI WA CHADEMA KUMUONA LISSU GEREZANI MPAKA KESI IISHE
Shahidi wa nne, Endrew Shabani Kamanyiro, mwenye umri wa miaka 57 na Mkristo kwa dini, alijitambulisha kuwa Mkuu wa Gereza Kuu la Ukonga. Katika ushahidi wake, alikiri kuwa ndiye mwenye mamlaka ya kusimamia shughuli zote za gereza hilo na kuwajibika kwa Kamishna Mkuu wa Magereza katika utekelezaji wa sheria, kanuni na usimamizi wa wafungwa.