Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the wordpress-seo domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /home/mwanzotv/public_html/wp-includes/functions.php on line 6114
Kamala Harris awasili Tanzania kuanza ziara yake ya siku tatu. - Mwanzo TV

Kamala Harris awasili Tanzania kuanza ziara yake ya siku tatu.

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris amewasili Dar es Salaam nchini Tanzania usiku wa Jumatano kwa ziara yake rasmi ya kiserikali ya siku tatu nchini humo

Alikaribishwa na Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Phillip Mpango katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Ndege ya Air Force Two, toleo maalum la C-32 ya Boeing 757-200 iliwasili Tanzania kutoka Ghana ambako Bi Harris alitumia siku tatu za kwanza za ziara yake barani Afrika. Pia anatarajiwa kuzuru Zambia kabla ya kusafiri kwa ndege kurudi Marekani.

Ziara hii ya kiserikali inatokana na mwaliko wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, wakati walipokutana jijini Washington mwaka 2022, ikitajwa pamoja na mambo mengine kuwa ni kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili, sambamba na kuzungumzia maendeleo ya uchumi, mabadiliko ya tabia nchi.

Wawili hao wakiwa na historia kwenye mataifa yao kuwa viongozi wanawake wa kwanza, watakuwa na mazungumzo na pia jioni atashiriki futari aliyoandaliwa na mwenyeji wake.

Marekani ni miongoni mwa mataifa yanayofanya vizuri kwenye uwekezaji nchini Tanzania ambapo hadi sasa miradi 266 ya Marekani imesajiliwa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ikiwa na thamani ya Dola 4.778 bilioni.

Itakumbukwa kuwa Ushirikiano wa Marekani na Tanzania ulianza mwaka 1961,na ilipofika mwaka 1968 nchi hizo ziliwekeana  saini kwenye  mikataba kadhaa ya ushirikiano na hadi sasa uhusiano huo unazidi kuimarika zaidi.