Waziri wa Madini nchini Tanzania, Dk. Doto Biteko, amesema Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imekwama kununua dhahabu kutokana na viwanda vya uchenjuaji madini nchini humo kutoanza kufanya kazi.
Dk. Biteko amesema kusuasua kuanza kazi kwa viwanda hivyo, kunaifanya dhahabu inayozalishwa nchini Tanzania kukosa ithibati za kimataifa.
Amesema BoT haiwezi kununua dhahabu ambayo haijasafishwa na kukidhi viwango vya kimataifa, ndiyo maana Serikali ilitafuta wawekezaji wa kujenga viwanda vya uchenjuaji, ambapo kwa sasa viko vitatu kwenye mikoa ya Mwanza, Geita na Dodoma.
“Ili ziweze kufanya kazi kuna taratibu za vibali mbalimbali vya kimataifa, vya kukuruhusu kusafisha. Wanakamilisha ithibati kwa maana mtu mwingine anaweza sema mbona viwanda vya uchenjuaji zipo lakini haijaanza, tunakamilisha taratibu za ithibati,”
Biteko ameongeza kuwa “ili waweze kutambua kimataifa, sababu ukichenjua bila ithibati madini yako ukiyasafisha hakuna atakayeyatambua. Utakuwa unacheza mchezo wa kuigiza, kwa hiyo hatua ya kwanza unajenga, unatafuta kibali, ukishapata dhahabu yoyote utakayoisafisha inatambuliwa kimataifa na unaweza kuiweka benki kama currency.”
Aidha amesema, viwanda hivyo vinakamilisha taratibu za ithibati ili vianze kufanya kazi ya uchenjuaji madini.
“Sasa baada ya uwepo wa refinery (usafishaji) hizo, sasa BoT hatakuwa na sababu nyingine za kununua dhahabu. Nia yetu nikwamba wanakamilisha taratibu zaoza ndani na tumekuwa tukikumbushana nao na wao wako tayari kununua,” amesema Biteko.
Serikali ya Tanzania imeendelea kudhibiti utoroshwaji madini, kwa kuweka mikakati mbalimbali, ikiwemo ya kuondoa urasimu kwenye utoaji vibali, licha ya kuwa bado vitendo hivyo vinaendelea