Waziri Nape asema hakuna wizi wa vifurushi vya simu unaofanywa na makampuni ya simu Tanzania

Waziri Nape ametoa kauli hiyo leo Mei 20,2022, alipokuwa akifanya majumuisho kwa wabunge waliochangia bajeti ya wizara yake, ambapo walilalimikia wizi unaofanywa na kampuni za simu katika huduma...

0
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari nchini Tanzania, Nape Nnauye

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari nchini Tanzania, Nape Nnauye, amesema uchunguzi uliofanywa ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini humo (TCRA), umebaini hakuna wizi wa vifurushi vya mawasiliano ya simu unaofanywa.

Waziri Nape ametoa kauli hiyo leo Mei 20,2022, alipokuwa akifanya majumuisho kwa wabunge waliochangia bajeti ya wizara yake, ambapo walilalimikia wizi unaofanywa na kampuni za simu katika huduma za bando na vifurushi.

“Bando ni nyongeza tu inayotolewa na mtoa huduma, ni huduma ya ziada, majirani zetu wanatumia ‘basic tariff’ kwa kuwa bando ni ndogo na ni huduma za ziada.

“Data moja inazalishwa kwa Sh 2.3 hadi Sh tisa,  hapa Tanzania tunauza kwa Sh 1.5 tunauza chini, sasa watoa huduma wakaona katika msingi ukitaka kutumia basic tariff itakuwa ghali…

“Sasa ukinunua tiketi kwenye basi ambayo unapaswa kutumia mwezi mmoja, ukatumia siku moja, halafu usisafiri tena, ndani ya mwezi mmoja je utaweza kuitumia tena? Hapana huwezi kuitumia tena.

“Lakini hapa tunavyoongea ni kama kuna wizi wizi wizi, ndio maana nilisema kama kuna mtu ana ushahidi aje.

“Vodacom, Tigo, Airtel ni nani anayekaa na kuamua tuibe data? hii fedha nani anachukua kwamba inaingia kwenye makampuni serious?

“Naomba Watanzania, TCRA imetoa press release nzuri, malalamiko yakapungua, nataka kutoa semina hapa kwa wabunge kisha tukae tuangalie hili,” amesema.

Hivi karibuni, Nape alitaja changamoto mbili kubwa kwenye matumizi ya simu janja ambapo, kwanza, mtumiaji anaweza kujiunga kifurushi cha intaneti, licha ya kuwa hatumii simu, kikapungua au kuisha kwa sababu kuna programu zinazoendelea kujiendesha kwenye simu.

Changamoto ya pili ni matumizi ya ‘hotspot’, ambapo uchunguzi wa TCRA umebaini kuna watu wamekuwa wakitumia huduma ya hotspot kwenye simu za watu wengine, hivyo kufanya vifurushi vyao kuisha kwa wakati.

Nape amesema elimu zaidi inahitajika juu ya matumizi ya intaneti na simu janja na kwamba, hakuna wizi wowote unaofanywa

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted