Search
Close this search box.
Africa

Alawiti mtoto wa miaka mitano kutokana na imani za kishirikina

8

Jeshi la Polisi mkoani Katavi, inamshikilia Juma Jackson (30), mkulima mkazi wa Kijiji cha Kagunga, Kata ya Kasekese, Wilaya ya Tanganyika kwa tuhuma za kumnajisi na kumlawiti binti mwenye umri wa miaka mitano.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, ACP Ali Makame Hamad, amesema tukio hilo lilitokea Juni 3, 2022, ambapo mtuhumiwa  anadaiwa kumvizia binti huyo njiani na kumkamata, kisha kutekeleza kitendo chake kwenye vichaka vilivyopo jirani na njia.

“Baada ya uchunguzi wa awali imebainika tukio hili linahusiana na imani za kishirikina, kwani mtuhumiwa aliahidiwa kulipwa ng’ombe watatu mara tu baada ya kutekeleza kitendo hicho, pia aende akamuoshee shambani kwake, ili iwe kama kizimba kwa ajili ya kuzindikia shamba,” amesema Kamanda huyo.

Kamanda amesema Polisi inaendelea na upelelezi wa tukio hilo na utakapokamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Comments are closed

Related Posts