Amuua mpenzi wake kisa wivu wa mapezi

Mkazi wa Kijiji cha Kiruru,Wialaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro amebakwa kisha kuawa kwa kukatwa katwa na panga shingoni na mwili wake  kutelekezwa kichakani kwa madai kuwa ni wivu wa mapenzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simoni Maigwa amesema  tukio hilo limetokea  Februari 24, 2022

“Huyu mwanamke alitoweka nyumbani kwao tangu Februari 21, taarifa zilitolewa katika kituo chetu cha Polisi Mwanga baada ya taarifa hii kutolewa upelelezi wa kina ulifanyika, hadi siku mwili wa marehemu ulipokutwa ukiwa porini kichakani ukiwa umeharibika huku shingo yake ikiwa imekatwa kwa kitu chenye ncha kali,”

Aidha Kamanda Maigwa amesema baada ya msako mkali kufanyika waliwakamata watuhumiwa wawili, akiwamo mpenzi wa binti huyo (marehemu) ambapo alikutwa na simu mbili za marehemu pamoja na mtuhumiwa wa pili ambaye alikutwa na panga.

“Katika mahojiano watuhumiwa hawa walikiri kutekeleza mauaji hayo ambapo walikiri kumbaka kabla ya kumuua mtuhumiwa wa kwanza (ambaye ni mpenzi wa marehemu)alikiri kupanga njama za kumuua mpenzi wake kwa kushirikiana na mwenzake ,”

“Kabla ya mauaji hayo ,mpenzi wa marehemu inadaiwa alikuta mawasiliano kwenye kwenye simu ya mpenzi wake(marehemu) akiwasiliana na mtuhumiwa wa pili ,ambapo baada ya kukuta mawasiliano hayo  alimtafuta mtuhumiwa wa pili  ambaye alikuwa akimtuhumu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na marehemu ndipo baada ya kukutana waliamu kula njama za kumuua binti huyo,”

Kamanda Maigwa amesema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani pindi taratibu za kisheria zitakapokamilika.