Mitandao ya Kijamii yafungwa nchini Mozambique katikati ya maandamano ya uchaguzi
Upatikanaji wa mitandao ya kijamii nchini Mozambique umekuwa na vizuizi kwa mara ya pili ndani ya wiki moja, taarifa kutoka kwa shirika la kimataifa linalofuatilia masuala ya mtandao ilisema, wakati upinzani ukitoa wito wa mgomo wa kitaifa kufuatia uchaguzi wa rais uliozua utata.