Kutoka Panya Road wa Dar hadi Panya Karoa wa Dodoma
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi nchini Tanzaniaimeahidi kuangamiza vikundi vya uhalifu vilivyoibuka katika Kata ya Makulu, jijini Dodoma vinavyojiita Panya Karoa.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi nchini Tanzaniaimeahidi kuangamiza vikundi vya uhalifu vilivyoibuka katika Kata ya Makulu, jijini Dodoma vinavyojiita Panya Karoa.
Mdee na wenzake wamekwenda mahakamani kupinga uamuzi wa chama hicho kwa kuwavua uanachama na wamefungua maombi Mahakama Kuu, dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema, wakiomba kibali cha kufungua shauri la mapitio ya kuhusu uamuzi huo.
“Nimeagiza hatua kali za kisheria zichukuliwe kwa kila aliyehusika na kueneza uongo kuwa TANESCO imepandisha bei ya umeme wakati wakijua fika sio kweli. Uenezaji wa taarifa za uongo kiasi hiki ni uchochezi wenye lengo la kujenga chuki dhidi ya TANESCO na Serikali”
Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, Patricia Kisinda, leo Ijumaa Juni 10, 2022 amewaachia huru washitakiwa hao baada ya kubaini kuwa ushahidi wa mashahidi 13 upande Jamhuri ulikuwa ukikinzana na pia hati ya mashitaka iliyosomwa mahakamani ilikuwa na kasoro nyingi.
Awali, Mei 31 mwaka huu Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Patricia Kisinda aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo, alipanga kutoa hukumu lakini ilishindikana kutokana na kudaiwa kuwa nje ya kituo cha kazi kwa majukumu mengine.
Jenerali Mabeyo alisema hayo juzi mkoani Morogoro wakati wa ziara yake ya kuaga vikosi vya ulinzi na usalama, pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Morogoro.
Nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa wameshiriki katika uchaguzi huo uliofanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ndani ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambapo nchi ya Msumbiji ilipigiwa kura 192, Ecuador – 190, Uswizi – 187, Malta- 185 na Japani – 184
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe alisema tukio hilo ni la Juni 4, mwaka huu na kijana huyo alikutwa amejinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali na tai ya shule.
Chanzo cha mauaji hayo ni mgogoro wa muda mrefu kati ya wanandoa hao hususani jioni mwanamke anapolewa na kuanza kumtuhumu mumewe kuwa hana msaada wowote katika maisha yao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, ACP Ali Makame Hamad, amesema tukio hilo lilitokea Juni 3, 2022, ambapo mtuhumiwa anadaiwa kumvizia binti huyo njiani na kumkamata, kisha kutekeleza kitendo chake kwenye vichaka vilivyopo jirani na njia.