Mawaziri wa Jinsia kutoka SADC wanatarajia kukutana kesho nchini Malawi
Kwa mujibu wa taarifa ya Sekretarieti ya Sadc kwa vyombo vya habari jana, mkutano huo utakaokuwa chini ya uenyekiti wa Waziri wa Jinsia, Maendeleo na Ustawi wa Jamii wa Malawi, Patricia Kaliati, utafuatilia utekelezaji wa Itifaki ya jumuiya hiyo kuhusu jinsia na maendeleo kwa kuzingatia nafasi ya wanawake katika siasa na utoaji uamuzi.