Ruto:Kenya kutoka kwenye dhiki ya deni.
Rais William Ruto amesema kwamba Kenya inatoka “katika dhiki ya madeni”, akipigia debe sera zake za kiuchumi licha ya hasira ya umma kuhusu nyongeza ya ushuru na kupunguza ruzuku wakati nchi hiyo ikiadhimisha miaka 60 ya uhuru wake.