Ocean Road waanza kutoa huduma ya urekebishaji wa mfumo wa nyongo iliyoziba pasipo upasuaji
Huduma hiyo mpya imeanza kutolewa hivi karibuni na Wataalam wa Radiolojia tiba wakiongozwa na daktari bingwa na mbobezi wa radiolojia tiba Dkt. Latifa Rajab kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road baada ya daktari huyo kurejea kutoka masomoni.