Masaibu ya wamaasai Ngorongoro yanazidi

Askari wa wanyama pori kutoka mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro siku ya jumanne waliingilia kikao cha wananchi wa Endulen tarafa ya Ngorongoro.

Photo Courtesy

kwa mujibu wakazi , tukio hilo ni kujaribu kuwazuia wananchi kupaza sauti zao kwa kunyimwa haki yao ya kupiga kura katika chaguzi zijazo.

 

Hivi karibuni tume ya taifa ya uchaguzi imetoa orodha ya vituo vya kupigia kura nchi nzima huku vituo vya kupigia kura katika tarafa nzima ya Ngorongoro zikikosekana kwenye orodha.

 

Kumekuwa pia na malalamiko kutoka kwa wananchi wa Ngorongoro kwamba, watu wote waliojiandikisha kupiga kura katika taarafa ya Ngorongoro kwenye chaguzi zilizopita sasa wanaonekana katika vituo vyao vya kupigia kura katika kijiji cha Msomera mkoa wa Tanga ambayo ni zaidi ya kilometa 500 kutoka Ngorongoro.