Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) imetangaza kumfungia kucheza ngumi Bondia Hassan Mwakinyo kwa kipindi cha mwaka mmoja na faini ya shilingi milioni moja.
Mwakinyo amepewa adhabu hiyo baada kugomea kupanda ulingoni September 29, 2023 katika pambano lake dhidi ya Julius Indonga kutokea Namibia kwa madai ya Promota kukiuka baadhi ya makubaliano yao..
Adhabu ya Mwakinyo inaanza leo Oktoba 10, 2023 hadi Oktoba 10, 2024.
Mwakinyo sasa ana siku saba za kukata rufaa dhidi ya adhabu hiyo.