Rais wa Somalia aitaka jumuiya ya kimataifa kuisaidia nchi yake kuepukana na njaa
Mashirika ya misaada yameonya kuhusu njaa huku visa vya utapiamlo miongoni mwa watoto vikiongezeka katika taifa hilo la Pembe ya Afrika
Mashirika ya misaada yameonya kuhusu njaa huku visa vya utapiamlo miongoni mwa watoto vikiongezeka katika taifa hilo la Pembe ya Afrika
Zaidi ya watu milioni 16.7 katika nchi hizo tatu wanakabiliwa na njaa kali huku idadi ikitarajiwa kuongezeka hadi milioni 20 ifikapo Septemba.
Wasomali milioni sita au asilimia 40 ya watu sasa wanakabiliwa na viwango vya juu vya uhaba wa chakula, kulingana na ripoti mpya ya Integrated Food Security Phase Classification
Mvua haijanyesha katika misimu ya mvua mitatu mfululizo huku eneo hilo likishuhudia hali ya ukame mbaya zaidi tangu 1981, shirika la Umoja wa Mataifa lilisema.