Mbowe afanya mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Tanzania
Mbowe amekutana na Balozi Battle ikiwa zimebaki siku 6 kuelekea maandamano ya amani yanayotarajiwa kufanyika Januari 24,2024.
Mbowe amekutana na Balozi Battle ikiwa zimebaki siku 6 kuelekea maandamano ya amani yanayotarajiwa kufanyika Januari 24,2024.
Chama Kikuu cha Upinzani nchini Tanzania, Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimesema tayari kimewasilisha barua kwa mamlaka za Polisi nchini humo juu ya kuzijulisha maandalizi yake ya kufanyika kwa Maandamano ya amani yatakayofanyika January 24 ambapo wameeleza kuwa maandamano hayo yatahitimishwa katika ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
Meli hiyo inayoitwa Norwegian Cruise Line Dawn yenye urefu wa mita 294, imetajwa kuwa kubwa zaidi kuwasili katika bandari zote nchini tangu kuanzishwa kwake. Norwegian Cruise Line Dawn ilianza kufanya kazi mwaka 2002 ikiwa na thamani ya zaidi ya Sh1 trilioni.
Msimamo huo umetolewa leo tarehe 15 Januari 2022 kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje Chadema, John Mrema, ikiwa ni siku moja baada ya Makonda kutaka mdahalo na viongozi wa chama hicho
Dk Nchimbi anachukua nafasi ya Daniel Chongolo ambaye alijiuzulu kwa kile alichodai kuwa amechafuliwa kwenye mitandao ya kijamii.
Mahakama ya kikatiba ya Uganda siku ya Jumatatu ilianza kusikiliza pingamizi la kwanza la sheria kali dhidi ya wapenzi wa jinsia moja ambayo imezua ukosoaji kutoka kwa Umoja wa Mataifa na kusababisha vikwazo vya viza vya Marekani kwa maafisa wa serikali.
Serikali ya Tanzania imetangaza kuyaunganisha mashirika na taasisi 16 na kufuta mashirika na taasisi za umma nne, ili kuongeza tija katika utendaji kazi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania January Makamba alitangaza Alhamisi Desemba 14, 2023 kuwa Serikali ya Israel iliwafahamisha kuwa Joshua Mollel, kijana wa Kitanzania aliyekuwa akisoma nchini Israel, aliuawa mara baada ya kuchukuliwa mateka na kundi la Hamas. tarehe 07 Oktoba 2023.
Mahakama Kuu ya Kanda ya Dar es Salaam jana Desemba 14,2023, ilibatilisha uamuzi wa Baraza Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) la kuwavua uanachama wabunge wa Viti Maalum, Halima Mdee na wenzake 18 ambao walituhumiwa kwenda Dodoma kuapishwa bila idhini ya chama hicho
Mganga mkuu wa Serikali nchini Tanzania, Prof. Tumaini Nagu amewata wananchi kuzingatia kanuni za afya kwa kuzingatia usafi na kupata chanjo ya UVIKO 19 kwa ukamilifu ili kujikinga na magonjwa ya njia ya hewa ikiwemo mafua, kikohozi, kupumua kwa shida, kuwashwa koo, homa na kuumwa kichwa.