Wagombea wanne wanaowania urais katika uchaguzi wa Kenya Agosti 9
Wagombea wanne wameidhinishwa kushiriki kinyang’anyiro cha kuwa rais wa Kenya, akiwemo naibu wa rais wa sasa William Ruto na Raila Odinga.
Wagombea wanne wameidhinishwa kushiriki kinyang’anyiro cha kuwa rais wa Kenya, akiwemo naibu wa rais wa sasa William Ruto na Raila Odinga.
Mgombea urais wa muungano wa Azimio Raila Odinga Jumatatu alizundua manifesto yake yenye ahadi 10, akiahidi kuinua uchumi ndani ya siku 100 za uongpzi wake kama Rais wa Kenya.
Uhuru, ambaye pia ni mlezi katika Muungano wa Azimio La Umoja One Kenya amemtaja Raila kama mtu bora zaidi kumrithi, kwa kile naibu wake Ruto amekitaja kuwa usaliti.
Wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Safari Park jijini Nairobi, Uhuru na Ruto walikaa kwa utulivu kila mmoja akishiriki kwenye meza yake tofauti.
Martha Karua huenda akawa naibu rais wa kwanza mwanamke katika historia ya Kenya, iwapo Muungano wa, Azimio la Umoja One Kenya, utashinda uchaguzi wa Agosti 9.
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka imetangaza kwenye gazeti la serikali majina 38 ya wagombea urais wanaotaka kuwania kiti cha urais katika uchaguzi wa Agosti kama wagombea binafsi.
Wakati Uchaguzi Mkuu unapokaribia, vyama vya siasa vinaharakisha kukamilisha mchujo wa vyama vyao kabla muda wa makataa Aprili 22,2022
Mahakama ya Upeo nchini Kenya iliamua Alhamisi kwamba pendekezo lenye utata la Rais Uhuru Kenyatta kufanya marekebisho ya katiba si halali
Jopo la majaji saba katika Mahakama ya Juu itafanya uamuzi kuhusu uhalali wa mapendekezo hayo kufuatia kukataliwa kwake na Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa