Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the wordpress-seo domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /home/mwanzotv/public_html/wp-includes/functions.php on line 6114
Watu 193 waliochangamana na wenye vurusi vya Murburg wawekwa karantini nchini Tanzania.  - Mwanzo TV

Watu 193 waliochangamana na wenye vurusi vya Murburg wawekwa karantini nchini Tanzania. 

Mganga Mkuu wa Serikali nchini Tanzania, Dk Tumaini Nagu amesema wagonjwa watatu waliogundulika kuwa na virusi vya Marburg wanaendelea na matibabu na hali zao zinaendelea kuimarika na hakuna maambukizi ya watu wengine tangu kuliporipotiwa kuzuka kwa virusi hivyo.

Dk Nagu ametoa taarifa hiyo jana mjini Bukoba ikiwa kama sehemu ya mwendelezo wa utoaji wa taarifa ya hali inayoendelea juu ya mlipuko wa virusi hivyo.

Ametaja mikakati ya Serikali juu ya  kupambana na ugonjwa huo kuwa ni pamoja na kuendelea kuelimisha wananchi jinsi ya kuweka kukabiliana na ugonjwa huo ambapo ni pamoja na watu  kunawa mikono na maji safi tiririka yenye sabuni.

Pia kutogusana mikono na kutoa taarifa kwa viongozi waliopo kwenye maeneo yao wanapobaini mtu mwenye dalili za kutapika au kutapika damu, kuharisha au kuharisha damu, kutokwa damu sehemu mbalimbali za mwili kuumwa kichwa na joto la mwili kupanda.

Aidha mkakati mwingine ni pamoja na kuweka vifaa vya kupima joto la mwili, vitakasa mikono na maji tiririka yenye sabuni maeneo yenye mikusanyiko ya watu kama vituo vya magari, maeneo ya soko kwenye viwanja vya ndege na bandarini na sehemu za biashara.

Aidha amesema watu wapatao 193 waliokuwa wamechangamana na watu waliobainika kuwa na ugonjwa wa Marburg mkoani hapa kati yao 89  wakiwa ni watumishi wa afya  wamewekwa karantini.

“Watu wapatao 193 ambao walichangamana na wagonjwa wa Marburg wamewekwa karantini na kati yao 89 ni watumishi wetu wa afya na tangu tumeanza kuwafuatilia hakuna mwenye dalili ya ugonjwa huu na tunaendelea kuwaangalia kwa karibu ndani ya siku 21,” amesema Dk Nagu.

https://mwanzotv.com/2023/03/23/tanzania-yaweka-mikakati-kudhibiti-homa-ya-marburg/