Waziri Mkuu mstaafu nchini Tanzania, aunganishwa kwenye kikosi kazi cha Rais Samia.

Waziri Mkuu mstaafu nchini Tanzania, Mizengo Pinda amejumuishwa kwenye kikosi kazi kilichoundwa na Rais Samia, kinachoendelea na shughuli ya kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa.

Pinda ambaye amewahi kuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya awamu ya nne nchini humo amejukuishwa leo kwenye Kikosi hicho kilichoteuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania, Jaji Francis Mutungi ikiwa mwezi mmoja sasa umepita tangu kuanza shughuli ya kukusanya maoni hayo.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi ilimshuhudia kiongozi hiyo akiwa ndani akitambulishwa rasmi mbele ya wajumbe wengine wanaounda kikosi tayari kwa kuendeleza shughuli.

Katika kikao hicho cha kumtambulisha kiliongozwa na Jaji Mutungi na baada ya mazungumzo ya kumtambulisha kiongozi huyo ilikuja Coaster nyeupe kumchukua akiambatana na baadhi ya viongozi akiwamo Profesa Rwekaza Mkandara ambaye ni mwenyekiti wa kikosi hicho.

Kwa mujibu wa mjumbe mmoja ambaye hakutaka jina lake kutajwa amesema kiongozi huyo amekuja kuongeza nguvu katika kikosi hicho.

“Amekuja kutambulishwa leo rasmi na tutakuwa naye hadi mwisho wa kukusanya maoni na kama umemuona anatoka hapa na baadhi ya wajumbe wameenda kuonana na Rais Ikulu,” amesema

Amesema kikosi hicho kuna wakati huwa kinaelemewa na hoja za wanaokuja kutoka maoni hivyo wanaamini uwepo wake na uzoefu wake watasaidia kuongeza utulivu.

Chanzo: Mwananchi