Wanaosambaza maudhui yenye viashiria vya ushoga nchini Tanzania waonywa
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari nchini humo, Nape Nnauye amesema Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imebaini kuwa baadhi ya watazamaji wa maudhui ya kulipia mtandaoni wamekuwa wakitazama na kusambaza maudhui hayo zikiwemo video kwenye mitandao ya kijamii.