East Africa Politics Tanzania

CCM yajitoa kuhusika na utekaji Tanzania, yataka ushirikiano na upinzani kukomesha utekaji nchini.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Emmanuel Nchimbi, amekanusha vikali madai kwamba chama chake kinahusika na matukio ya utekaji na mauaji yanayoendelea nchini Tanzania. Nchimbi alisisitiza kuwa vitendo hivi vinachochewa na magenge ya uhalifu yenye lengo la kutafsiri CCM kama wauaji na  kuchochea ugumu wa uhusiano kati ya chama hicho na wananchi.